Neymar anatazamia kuondoka Saudi Arabia na amewaambia wachezaji klabu yake ya zamani ya Santos kwamba atarejea Brazil ifikapo mwaka 2025, kwa mujibu wa ESPN.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 32, aliondoka Paris Saint-Germain na kujiunga na Al Hilal msimu wa majira ya joto kwa dau la euro milioni 90, lakini akaumia kwenye mechi tano tu katika maisha yake ya soka nchini Saudi Arabia.

Mkataba wake unaaminika kuwa na thamani ya karibu euro milioni 150 kwa msimu.

Huku akiwa hayupo, Neymar alirejea Brazil kuitazama timu yake ya zamani ya Santos ikimenyana na Palmeiras katika fainali ya Campeonato Paulista, na kwa mujibu wa UOL Esporte, ndipo alipotangaza kwa faragha mpango wake wa kuondoka Saudi Arabia.

Neymar anaripotiwa kuwaambia wachezaji na wafanyakazi wa Santos kwamba anapanga kucheza katika msimu wa 2025 wa Brazil, ambao unatarajiwa kuanza Aprili 2025 miezi miwili kabla ya mkataba wake na Al Hilal kumalizika.

Winga huyo aliwahi kuzungumzia nia ya kurejea Brazil wakati fulani, sasa ni dalili kwamba Neymar ana mpango wa kuondoka Saudia.

Neymar alionesha kiwango kizuri katika wiki za mwanzo za muda wake nchini Saudi Arabia, akitengeneza pasi tatu za mabao na kufunga katika mechi tano kabla ya kuumia.

Licha ya kukosekana kwake, Al Hilal wamebakia kileleni mwa msimamo wakiongoza kwa pointi 12, wakiongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Fulham, Aleksandar Mitrovic aliyefunga mabao 22.

Sergej Milinkovic-Savic na Ruben Neves wanaongoza katika chati za wasaidizi wa klabu hiyo, huku winga wa zamani wa Barcelona, Malcom pia akiwa amefunga mabao 14 na kutoa pasi za mabao kumi katika michuano yote.

Al Hilal wanatarajiwa kuwika msimu huu wa majira ya joto na wanatarajiwa kushinikiza kumsajili Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, ambaye analengwa zaidi na Saudi Pro League pamoja na kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne.

Maumivu ya kichwa yamvuruga Varane
Man Utd kuibomoa Southampton