Mabeki wa Manchester United, Lisandro Martinez na Victor Lindelof wote watakuwa nje kwa angalau mwezi mmoja kutokana na majeraha ya misuli waliyoyapata siku za hivi karibuni.
Klabu hiyo ilithibitisha pigo hilo la majeruhi hao wawili katika taarifa yake usiku wa kuamkia leo.
Lindelof alipata jeraha la misuli ya paja wakati wa sare ya 1-1 Jumamosi dhidi ya Brentford kwenye Ligi Kuu England, huku raia huyo wa Sweden akishindwa kumaliza pambano hilo Magharibi mwa London.
Martinez alichukua nafasi ya Lindelof baada ya dakika 69 za mchezo katika kurejea kwake kutoka kwa malalamiko ya awali ya goti. Lakini baada ya kucheza mechi yake ya kwanza tangu Februari, mwaka huu, alijikuta akijitonesha na hivyo kumlazimisha naye kuwa nje ya Uwanja.
Beki huyo wa kati wa zamani wa Ajax aliumia katika mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Sevilla Aprili mwaka jana, na kumlazimu kukosa mwisho wa msimu. Baadae alikuwa na wakati mbaya zaidi Agosti na akacheza mechi kadhaa kabla ya kuondolewa uwanjani hadi Januari. Alianza mara tatu tu, kabla ya tatizo la goti la Februari. Raphael Varane alitolewa wakati wa mapumziko dhidi ya Brentford kama tahadhari.
Kutokuwepo kwake kwenye taarifa ya United kuhusu Martinez na Lindelof kunaweza kuwa dalili ya Mfaransa huyo kutokuwa na wasiwasi mkubwa. Jonny Evans pia alikosekana kwenye kikosi Jumamosi kutokana na jeraha.
Kwa jinsi mambo yalivyo, Harry Maguire ndiye beki pekee wa kati mwandamizi ambaye yuko fiti na anayepatikana kabla ya safari ya United kurejea London kumenyana na Chelsea baadae leo Alhamis (Aprili 04).
Luke Shaw pia kwa sasa hayupo kutokana na jeraha. Varane au Evans bado wanaweza kuwa katika kinyang’anyiro cha mchezo huo dhidi ya Chelsea.
youtube.com/watch?v=tFXsOvozSMY&t=798s