Klabu ya Newcastle United imerejea tena kutaka kumnunua mlinda mlango wa Arsenal, Aaron Ramsdale, ripoti mpya imedai.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amepoteza nafasi yake kwenye Uwanja wa Emirates kwa David Raya, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Brentford, baada ya kukaa kwa misimu miwili kama kipa chaguo la kwanza wa klabu hiyo.

Chelsea imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa na Ramsdale, ambaye alichukua jukumu muhimu katika harakati za Arsenal kuwania taji la Ligi Kuu England msimu uliopita, lakini 9Omin ilifichua mwishoni mwa Februari haiwezekani kuhamia Stamford Bridge katika hatua hii.

West Ham United pia imekuwa ikimfuatilia Ramsdale, ambaye anatarajiwa kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake baada ya Euro 2024 msimu huu wa joto huku kukiwa na nia ya klabu nyingine kutoka Ulaya.

Tovuti ya 90min imeeleza kuwa Ramsdale, ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 2021 kwa dili la pauni million 30, angependelea kubakia katika Ligi Kuu England, na Mail Sport iliripoti Newcastle inaweza kumpa njia nyingine kutoka London Kaskazini wakati wanataka kuimarisha kikosi chao.

Kocha, Eddie Howe, tayari amemsajili Ramsdale mara moja katika maisha yake ya soka, wakati akiwa Bournermouth, na inadaiwa mipango ya uhamisho ya Newcastle ni pamoja na kuleta mbadala wa makipa wawili, Martin Dubravka na Nick Pope.

Dubravka (35), kwa sasa anamiliki glavu huko Tyneside, huku Pope (32), akiendelea kupata nafuu kutokana na bega lake lililoteguka wakati wa mechi iliyofanyika Desemba mwaka jana dhidi ya Manchester United, lakini mkataba wa Mslovakia huyo una zaidi ya mwaka mmoja tu kukamilika.

Ramsdale ameichezea Arsenal mechi sita pekee za Ligi Kuu England msimu huu baada ya kuwasili kwa Raya.

Mikopo: Atakayeunda kikundi hewa amejifukuza kazi - Mchengerwa
Afariki kwa kudondokewa na ukuta Moro