Johansen Buberwa – Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajath Fatma Mwasa amekemea vikali na kuyatahadhalisha makundi ambayo huchochea wenzao kuanzisha vurugu zisizokuwa na tija, huku aklida anazo taarifa za kutosha kuhusiana na makundi hayo na Serikali haitosita kuchukua hatua kali za kisheria juu yao.

Mwasa ameyasema hayo katika kikao maalum kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera na kufanya mazungumzo na Maimamu wa Misikiti Kutoka Madhehebu ya Dini ya Kiislamu Wilayani Bukoba.

“Nawasisitiza Viongozi kuendelea kuitunza Amani, kujiepusha na Vitendo vyote vyenye kuashiria uvunjifu wa Amani, wakiwemo wale wanaogombea Uongozi na kwa sasa Serikali ya mkoa itakuwa tayari kumchukulia hatua  yeyote atayejaribu kufanya Vitendo vya uvunjifu wa Amani kwa kutumia mwavuli wa dini bila kujali dhehebu lake Wala Taasisi yake,” alisema.

Katika hatu nyingine, RC Mwassa alitoa Sadaka ya Ifutar kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa  Kagera kwa Viongozi hao ambao alidai wana mchango mkubwa hasa katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Iftar ya Dkt. Rweikiza: Jamii ikumbukwe kipindi chote - Baitu
Simba SC yamshughulisha Kocha Mashujaa FC