Hii leo Aprili 7, 2024 Rwanda inaadhimisha miaka 30 tangu kufanyika kwa mauaji ya kimbari, ambapo karibu watu 800,000 waliuawa.
Maadhimisho haya yanawadia huku makaburi ya halaiki yakiendelea kugundulika hadi sasa katika nchi hiyo yenye watu karibu milioni 14.
Viongozi mbalimbali akiwemo aliyekuwa rais wa Marekani wakati wa mauaji hayo Bill Clinton wanatarajia kuhudhuria maadhimisho hayo.
Tayari Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit ambaye pia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki – EAC, amewasili nchini Rwanda kwa ajili ya kumbukumbu hiyo ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi.