Maisha ni kupanda, lakini kuwa na mtazamo wa pande zote ni jambo la muhimu kwani kuna wakati mambo huenda kombo na usione uhalisia wa kufanikiwa na ukaka chini ukihisi safari yako imefikia ukingoni.
Hali kama hiyo tunaita ni kukata tamaa, lakini ipo misemo ambayo inaweza kukufanya ukanyanyuka tena kupambana upya na ukapata matokeo chanya kiasi ukajutia muda ulioupoteza kwa kukaa chini.
Ni maneno ya kutia moyo yanayoweza kukusaidia, pia yakakukumbusha namna ya kuishi maisha kwa ukamilifu na ustahimilivu kupitia changamoto zozote zinazokuja mbele yako.
Ikiwa unafahamu au hufahamu basi hapa upo usaidizi wa baadhi ya nukuu kuhusu maisha zinazodumu katika miongo yote, kwani kila mafanikio ya mtu hutokana na mtu mwenyewe.
Elewa kwamba MUNGU hakukuumba uwe masikini, vyote walivyonavyo wanadamu hawakuzaliwa navyo walipambana, hivyo nawe muda umefika USIKAE CHINI KUNGOJA MAFANIKIO, NYANYUKA:
Karibu kusoma nukuu hizi 10 na ziada kisha itilie maanani, ili iwe msaada kwako katika siku zijazo kwenye safari yako ya kutafuta ushindi wa maisha katika nyanja zote.
1. “Unaweza kumbana na changamoto nyingi maishani, lakini kamwe usijiruhusu kushindwa.” Maya Angelou.
2. “Maisha ni somo refu la unyenyekevu.” – J.M. Barrie.
3. “Kuishi ni jambo adimu zaidi duniani. Watu wengi wapo, hivyo tu.” – Oscar Wilde
4. “Jambo muhimu zaidi ni kufurahia maisha yako – kuwa na furaha – yote ni muhimu.” – Audrey Hepburn.
5. “Ili kufanikiwa maishani, unahitaji vitu vitatu: matamanio, uti wa mgongo na mfupa wa kuchekesha.” – Reba McEntire.
6. “Lazima tuwe tayari kuachana na maisha tuliyopanga ili tuwe na maisha ambayo yanatusubiri.” – Joseph Campbell.
7. “Maisha ni mfululizo wa masomo ambayo lazima uyaishi ili kueleweka.” Ralph Waldo Emerson.
8. “Penda maisha unayoishi. Ishi maisha unayopenda.” Bob Marley.
9. ‘Penye nia Pana njia, usikate tamaa pambania nia yako.” Mathew Mbalina.
10. “Mchumia juani hulia kivulini, subira yavuta heri, mtarazaki hachoki na riziki ya mbwa ipo miguuni pake.” Wahenga.