Kamanda wa Polisi Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Allan Bukumbi amethibitisha kukamatwa kwa Watu 16 Raia wa Ethiopia waliokuwa wakisafirishwa kwa kutumia gari aina ya Toyota Land Cruiser V8, katika eneo la Msitu wa Lunganga kata ya Sao Hill.
Kmanda Bukumbi amesema, zoezi hilo lilifanikiwa kwa ushirikiano wa Jeshi la polisi Mkoani Iringa na Jeshi la uhamiaji, ambapo watu hao walikamatwa katika msitu huo uliopo Tarafa ya Ifwagi Halmashauri ya mji wa Mafinga Wilayani Mufindi Mkoani Iringa.
Amesema, Wahamiaji hao wasio na vibali walitekelezwa katika mashamba ya Mahindi baada ya kushushwa kwenye gari ambalo awali lilisomeka kwa namba bandia za STL 3999 ambapo Dereva wa gari hilo alitekeleza pia gari hilo na kutokomea kusikojulikana.
Kamanda Bukumbi amesema uchunguzi wa awali umeonesha kuwa gari hilo lilikuwa limesajiliwa kwa namba T 803 CVW likimilikiwa na Said Hassan mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam.
Hili linakua gari la tatu aina ya Land Cruiser V8 kukamatwa likiwa na Wahamiaji wasio na vibali ambapo mengine mawili yalikamatwa ndani ya siku 15 zilizopita Mkoani Manyara.