Katika kipindi cha miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki imeendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya miundombinu ya uchukuzi, maji na nishati kutoka Serikali ya Japan, inayotokelezwa na JICA Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijiji Dodoma Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Africa mashariki, Mbarouk Nassor amesema Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na Development of Malindi Fish Landing Marketing wa Zanzibar wenye thamani ya takribani Tshs bilioni 19.610 uliokamilika mwaka 2023, Improvement of Transport Capacity wa Jijini Dar es Salaam uliogharimu  Bilioni 22.482 uliokamilika mwaka 2023.

“Lakini pia na mradi wa upanuzi wa barabara mpya ya Bagamoyo awamu ya pili Kipande cha Moroco – Mwenge chenye ukubwa wa Km. 4.3 uliogharimu takribani Tshs bilioni 81.350. Mradi wa usambazaji maji mjini Zanzibar uliogharimu takribani Tshs bilioni 217.3 ulioanza mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2027,” alisema Mbarouk.

Hata hivyo, amesema Katika kuimarisha ushirikiano wa uwili Tanzania na nchi marafiki zimekuwa zikitafuta ufumbuzi wa Vikwazo Visivyo vya Forodha (NTBs) kwa lengo la kuimarisha biashara.

“Mathalan, kuanzia mwaka 2007 mpaka 2023 Tanzania na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimefanikiwa kuondoa zaidi ya vikwazo 309  vinavyo athiri biashara katika nchi zao”,amesema

Balozi Mbarouk ameongeza kuwa, Tanzania imefanikiwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa dhana ya kutatua changamoto za kidunia kwa pamoja yaani Multilateralism.

“Na Katika eneo hili, Tanzania imefanikiwa kuwa mbia anayeaminika na kukubalika katika maamuzi mbalimbali duniani hasa katika mashirika ya kimataifa hususan Umoja wa Mataifa.”

“Katika kutekeleza hili Tanzania imekuwa ni mbia katika maamuzi kwenye vyombo mbalimbali ikiwemo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, Benki ya Dunia, Shirika la Biashara Duniani (WTO),” amesema Mbarouk.

Binti ajifungua mapacha kambi ya Waathiriwa mafuriko
JWTZ watoa magari kuhudumia waathiriwa wa mafuriko