Watoto mapacha wa kiume wamezaliwa kwenye kambi ya Waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji huko Wilayani Kibiti Mkoani Pwani.

Hilo limefahamika wakati ikitolewa hali ya athari za mafuriko katika Wilaya ya Kibiti kwa uongozi wa UWT Taifa, Mary Chatanda aliyetembelea na kuzungumza na waathirika wa mafuriko wa Wilaya za Kibiti na Rufiji Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Korombo.

Amesema, Mwanamke aliyejifungua Kambi ya wahanga Mafuriko Mtomboli Kibiti ni Sabrina Khamisi Mwanzalima (19), Dini Muslim aliyejifungua Aprili 10, 2024.

Kanali Korombo alisema watoto hao mapacha kwa mama huyo ni uzao wake wa kwanza na wote wanaendelea vizuri.

Aidha Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda alimpongeza mama huyo na akutoa viaa maalumu kwa mama huyo aliyejifungua watoto mapacha.

Nabi, Robertinho watia neno Kariakkoo dabi
Balozi Mbarouk ataja mafanikio miradi ya maendeleo