Maonesho ya Biashara yamezinduliwa hii leo Aprili 19, 2024 katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam ikiwa ni harakati za kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania yanayotarajia kufikia kilele chake Aprili 26, 2024.

Mgeni rasmi katika uzinduzi, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulah amesema maonesho hayo ni sehemu ya kuendeleza Muungano na pia ni fursa kubwa ya kuutangaza kwa mataifa mengine duniani.

Amesema, “kwa miaka 60 tumefanikwa kuulinda na kuudumisha muungano huo, tofauti na mataifa mengine mengi yameshindwa kuwa na muungano imara, Mtanzania mwenye akili timamu hawezi kuongea vibaya kuhusu muungano.”

Aidha, amewapongeza waandaji wa maonesho hayo, huku akitoa Salaam za Rais Samia kwa Watanzania wote kuulinda na kuendeleza Muungano huo kwa gharama yoyote.

Maonesho hayo ambayo yameratibiwa na Mamlaka ya maendeleo ya Biashara Nchini – TANTRADE, yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, Wafanyabiasha, Wadau na Wananchi.

Tanganyika wapanda miche 1,050 iliyo hatarini kutoweka
TAWA yawasaka Mamba tishio kwa Binadamu