Afisa wa ngazi ya juu wa Iran, amesema kuwa nchi hiyo haina mpango wa kulipiza kisasi kwa kile kinachoelezwa na vyanzo vya habari kuwa shambulizi la Israel katika mji wa Isfahan Aprili 19, 2024.

Afisa huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja amenukuliwa akisema kilichotekea ni hujuma za kujipenyeza kuliko kuwa mashambulizi yanayoripotiwa na vyanzo vya kigeni.

Naye Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Hossein Amirabdollahian amesema mashambulizi yalifanywa na dronindogo na hayakusababisha uharibifu wowote.

Hata hivyo, Israel bado haijatoa taarifa yoyote juu ya mashambulizi hayo inayoripotiwa kuyafanya, na mshirika wake mkuu, Marekani imekataa kujihusisha.

Ajali iliyouwa Mkuu wa Majeshi: Timu ya uchunguzi yaundwa
Dkt. Nchimbi asisitiza uadilifu, uwajibikaji mali za umma