Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, Kipchumba Murkomen ameteua timu ya uchunguzi kufuatia ajali ya helikopta iliyomuua Mkuu wa Jeshi, Jenerali Francis Ogolla na wanajeshi wengine tisa wa KDF.

Kupitia notisi ya gazeti la Serikali, Murkomen ameibainisha kuwa timu hiuo itakayoongozwa na Kapteni Peter Maranga itakagua ripoti zote za ajali zinazohusisha ndege za Kenya.

Ripoti hizo ji zile zilizowasilishwa na Jamhuri ya Sudan Kusini na Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia katika miaka mitano iliyopita.

Kenya ilitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, baada ya vifo vya maafisa 10 wakuu wa jeshi akiwemo mkuu huyo wa majeshi, Jenerali Francis Ogolla.

Mama Mariam: Serikali inawathamini Wanawake
Iran: Hatuna mpango wa kulipiza kisasi