Mabosi wa Real Madrid wamepanga kusubiri hadi mwaka 2025 kabla ya kumsajili beki wa kushoto kutoka nchini Canada na klabu ya Bayern Munich, Alphonso Davies, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kuona kuna ugumu kumpata katika dirisha lijalo.
Davies mwenye umri wa miaka 23, anadaiwa kukataa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Bayern na kuwaambia kwamba anataka kuondoka.
Hata hivyo, Bayern haionekani kuwa tayari kumuachia fundi huyu mwisho wa msimu kwani bado ina matumaini ya kumsainisha mkataba mpya licha ya ugumu uliopo.
Madrid imekuwa ikihitaji huduma ya staa huyu kwa muda mrefu kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ulinzi ambapo hadi leo bado inaona haijapata mbadala wa Marcello.
Tangu kuanza kwa msimu huu 2023/24 Davies amecheza mechi 34 za michuano yote.