Swaum Katambo – Tanganyika.

Watanzania wametakiwa kudumisha amani ya Nchi ili kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kama ilivyokuwa dhumuni la waasisi wa muungano huo Mwl. Julius Nyerere na Abeid Aman Karume.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu wakati wa sala na dua ya kuliombea Taifa na kuadhimisha sherehe za Muungano wa Tanzania, ibada iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mpanda ndogo.

Amewataka vijana kufahamu historia ya nchi ilipotoka,ilipo na inapokwenda ili kuacha tabia za kubeza maendeleo yanayofanywa na serikali.

Hotuba hiyo imetolewa baada ya maombi ya kuliombea Taifa kutoka kwa viongozi wa dini mbalimbali.

Rais Samia aridhishwa kazi za Mabalozi, ataka juhudi zaidi
Cole Palmer kufungua ukurasa mpya Chelsea