Lydia Mollel – Morogoro.
Katika jitihada za kuzuia na kupambana na rushwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Mkoani Morogoro imewataka wakandarasi wanaowasilisha wasifu wa uongo kwenye miradi mbalimbali kwa lengo la kujipatia kazi kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume na sheria.
Akizungumza mkoani hapo, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Christopher Mwakajinga amesema Takukuru mkoa wa Morogoro imebainisha kuwa baadhi ya wakandarasi wanawasilisha taarifa za uongo nakupelekea miradi mingi kukwama au kuchelewa kukamilika.
Aidha, amewataka Wananchi kuwa makini pindi wanapoweka pesa kwa mawakala kwani badhi yao wanachapisha stakabadhi Batali na kuwaibia
Hata hivyo, TAKUKURU imewata wananchi kutoa taarifa ya vitendo vya rushwa lakini pia imewashukuru wananchi wote waoendelea kutoa ushirikiano dhidi ya vitendo hivyo na kuwaimiza kutembelea ofisi Takukuru zilizopo wilaya zote za Morogoro.