Swaum Katambo – Katavi.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Mkoa wa Katavi wamefanikiwa kukisaidia Kijiji cha Ibindi kupata malipo waliyopaswa kulipwa tangu mwaka 2016 ya shilingi 300,000 kwa mwezi bila VAT, kwenye akaunti ya Kijiji kufuatia mnara uliojengwa katika Kijiji hicho na Kampuni ya Tigo Tanzania.
Akitoa taarifa ya kipindi cha Januari hadi Machi, 2024 kwa Waandishi wa Habari Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi, Faustine Maijo amesema wamefanikisha hilo kupitia Programu ya TAKUKURU RAFIKI kwa kushirikiana na uongozi wa Halmashauri ya Nsimbo.
Amesema, Kijiji cha Ibindi kitapokea malipo yote ya kipindi ambacho yalikuwa hayajafanyika tangu mwaka 2016.