Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA),imesaini mkataba wa makubaliano wa shilingi bilion 40 na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),kwa ajili ya kusaidiana katika maeneo matatu .
Maeneo hayo makubwa matatu ni pamoja na kuwajengea uwezo katika Ununuzi wa Umma, kuwajengea uwezo wadau wakiwamo wakandarasi na eneo la tatu ni kuwezesha mamalaka hiyo kupata vitendea kazi.
Akizungumza leo April 24, 2024 jijini Dodoma mara baada ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Eliakim Maswi amesema Mamlaka hiyo imeingia mkataba huo ili kuwezeshwa kuwa na vitendea kazi.
Maswi ameeleza PPRA inashughulika na ukaguzi wa thamani hali ya fedha zinazotumika katika nchi na kwamba hawawezi kupewa vifaa kabla hawajasaini mkataba.
Ameongeza kuwa makubaliano hayo walianza kujadili mwaka 2022 ambapo yalipita katika Wizara ya fedha na Tume ya mipango na baadae yakakubalika kwa ajili ya kusaidiana.
Amesema kuwa UNDP ni ya ulimwengu hivyo kutokana na kufanya manunuzi makubwa katika ulimwengu ni vizuri nao wakasaidia ili kujiimarisha katika eneo la kujenga wa taasisi na uwezo wa watu ambao wanahusika na Ununuzi wa Umma.
Sheria yao ya Ununuzi wa Umma ilipitisha mwaka jana moja ya eneo ambalo walijadili na wabunge ni kuwezesha wazawa kutumika kusimamia miradi mikubwa nchini huku akisema sheria hiyo inasema miradi yote ambayo ni chini ya bilioni 50 lazima iwe ya wazawa.
“Kama kuna mradi wenye ukubwa zaidi ya hiyo lazima kampuni itakayosimamia, kuongeza lazima iwe ya wazawa pia ili kampuni za wageni zihamishe utaalumu walionao kuja kwa wazawa hivyo UNDP wamekubali kutujengea uwezo wakandarasi wetu wadogo ili waweze kuwa na uwezo wa kufanya kazi vizuri, “amesema.