Aprili 25 kila mwaka ni siku ya Malaria Ulimwenguni, ambapo Shirika la Afya duniani – WHO, hutoa elimu kuhusu juhudi za pamoja na kujiepusha na malaria katika Mataifa, huku ikikadiriwa kuwa kuna zaidi ya visa milioni 240 vya malaria kila mwaka na vifo vya zaidi ya watu 400,000 katika nchi 60 kila mwaka.
WHO inasema, mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko la viwango vya joto husababisha ugonjwa huo hatari unaweza kusababisha kifo kuweza kusambaa katika maeneo mengine mapya katika Ulimwengu ambako awali ambako haukuwahi kuwepo.
Hata hivyo, mabadiliko ya tabia nchi pia yanaweza kupunguza kusambaa kwa malaria katika baadhi ya maeneo ambako tayai hali ilikuwa mbaya zaidi, hivyo uwepo wa uelewa wa athari za mabadiliko ya hali ya joto litakuwa ni jambo muhimu katika kuendeleza mapambana dhidi ya ugonjwa huo.
Malaria ni ugonjwa hatari unaosambazwa nna mbu, ambao unaweza kusababisha kifo iwapo haukubainika na kutibiwa mapema na dalili zake ni pamoja na joto la juu, kutoka jasho, kuhisi baridi, maumivu ya kichwa, kuchoka, kupoteza hamu ya kula, maumivu ya mwili.