Scolastika Msewa – Rufiji.

Taasisi ya Elimu Tanzania, TET imekabidhi vitabu vya kusomea 422 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 7 kwa ajili ya Shule tatu zilizofungwa kwa kuathiriwa na mafuriko ya Mto Rufiji, Wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Hemed Magaro kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph kolombo, Mkuu wa kitengo Cha Elimu maalumu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt. Magreth Matonya alisema vitabu hivyo ni kwa Shule ambazo watoto wamefunga na vifaa vyao vyote vilichukuliwa na maji ya mafuriko.

Alisema, awali walileta vifaa vyote vya kujikimu mtoto katika kujisomea lakini TET wameleta vitabu vya kusomea ambavyo vitasaidia Mwalimu na mwanafunzi waweze kufundishana kwenye mahema au kwenye Shule maalumu zilizochaguliwa kwaajili ya kuwastili watoto walipata changamoto za mafuriko.

Dkt. Matonya alisema Kuna vitabu 121 vya Delta shule ya msingi, vitabu 181 vya Usimbe shule ya msingi, vitabu 122 vya Shule ya msingi Nyambele.

Naye Mfanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania TET John Ngowi alisema walipokea maelekezo ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Aldof Mkenda na wameleta vitabu hivyo kwaajili ya Wanafunzi walioshindwa kuhudhuria vipindi vya masomo yao kwasababu ya mafuriko ya Mto Rufiji yaliyowakuta na kuzoa vitatu vyao.

Alisema vitabu vilivyoletwa ni vya kufundishia kwa madarasa yote ya msingi kwa Shule hizo tatu vyenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 7 na Taasisi hiyo bado ipo tayari kuendelea kushirikiana na Wilaya hiyo kutatua changamoto hiyo.

 

PPRA, ZPPDA wasaini mkataba wa makubaliano