Mshambuliaji wa FC Bayern Munich, Harry Kane, amejiwekea rekodi yake bora zaidi baada ya kufikisha mabao 42 katika michuano yote wakati akifunga mawili dhidi ya Eintracht Frankfurt huku Jumamosi iliyopita akiiwania ile ya Robert Lewandowski ya kufunga mabao mengi kwa msimu mmoja.
Kane ameipita rekodi yake ya mabao yake bora zaidi (mabao 41) aliyoiweka Tottenham msimu wa 2017-18.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa England ambaye alijiunga na Bayern majira ya joto yaliyopita, sasa anawania rekodi ya Lewandowski ya kufunga mabao 41 kwa msimu mmoja kwenye Bundesliga, huku Kane akihitaji mabao sita zaidi katika mechi tatu zilizosalia za Bayern.
“Inawezekana, lakini ni wazi lazima nipate hatua,” alisema Kane alipoulizwa kama anaweza kufikia rekodi ya Lewandowski.
“Labda nifunge mabao machache wiki ijayo. Iko pale, iko umbali wa kugusa.”
Uchezaji wa Kane wa nyumbani unakuja wakati wa msimnu mgumu huko Bayern ambao umewafanya kushindwa kunyanyua taji la Bundesliga kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 12 na kukumbana na kipigo cha kufedheha cha Kombe la Ujerumani kufuzu kwa raundi ya tatu mikononi mwa Saarbrucken ya Daraja la Tatu.
Hata hivyo, Bayern bado wanaweza kuokoa msimu wao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwalaza Arsenal katika Robo Fainali mapema mwezi huu, na kuifuata Real Madrid Nusu Fainali.
Mechi ya mkondo wa kwanza itachezwa leo Jumanne (Aprili 30) kwenye Uwanja wa Allianz Arena.