Mabadiliko Mfumo wa elimu yametajwa kuwa ni chachu katika kuchangia, kumaliza au kupunguza rushwa ya ngono ambayo imekuwa ikisababisha matatizo kwa Wasichana kwa kuathiri maendeleo na haki zao hasa wale walio katika vyuo vya elimu ya juu.
Akozungumza na Dar24 Media, Mdau wa Elimu na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Soma Kitabu – SK, Adam Mbalina amesema wito wake kwa Serikali ni kuona inafanya mabadiliko katika eneo hilo, ili kumlinda mtoto wa kike dhidi ya rushwa ya ngono.
Amesema, mfumo uliopo unatoa mianya ya rushwa kwa Walimu wa Wasichana wa ngazi huyo na kwamba sheria zilizopo huwalinda Walimu pale inapogundulika uwepo wa suala la rushwa ya ngono huku jamii ikishindwa kupatia mtoto wa kike elimu na kutatua changamoto zinazomkabili wakati wa akitafuta elimu.
“Kiufupi mfumo uliopo unampa Mwalimu uwezo wa kumbana Mwanafunzi anaposhindwa kufaulu masomo yake hilo la kwanza lakini pia ninaiomba Serikali iangalie uhuru iliowapa Wanachuo kwani wengi wao huutumia vibaya kwa kuvaa mavazi yasiyo na maadilili.”