Mei 3 kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, ambapo uhalisia unaonesha hali ya Vyombo vya Habari si nzuri kimaudhui, kifedha, na kiteknolojia.
Na ili kuepukana na ufikiaji wa hali mbaya zaidi ni wazi kuwa Vyombo vya Habari vinatakiwa viwekeze kwenye teknolojia na waandishi kuongeza ujuzi, ili kuendana na wakati huku fedha ikitafutwa.
Aidha, sote tunatambua ujio wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka huu 2024 na ule mkuu wa 2025, katika hili Vyombo vya Habari poa vinatakiwa kutoa nafasi sawa kwa vyama vya siasa katika kuripoti matukio mbalimbali.
Nchini Tanzania maadhimisho haya pia yanafanyika ambapo kwa siku ya kwanza Spika wa Bunge, Tulia Ackson alikuwa mgeni rasmi na alikazia kwa kusisitiza ufuatiliaji wa taasisi za serikali zinazodaiwa fedha na vyombo vya habari, ili walipe madeni yao na vyombo viweze kujiendesha.
Leo Machi 3, 2024 ni kilele cha siku hii muhimu kwetu, mgeni rasmi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, tunataraji kuna jambo ataliongea ingawa tayari Waziri mwenye dhamana ya Habari Nape Nnauye amesema jambo.
Namnukuu, “hali ya uhuru wa vyombo vya habari katika nchi yetu inaendelea kuimarika, hatujafika tunakotaka kwenda lakini kwa hakika hatupo tulipokuwa jana, mazingira ya jana na leo ni tofauti na wanahabari wanakubaliana na mimi, tumefika hapa kwenye maboresho haya yaliyofanyika kwa sababu ya utashi wa kisiasa wa serikali.”