Scolastica Msewa – Kibiti.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava amekemea tabia ya baadhi ya watu kwenye jamii kuwabagua na kuwanyanyasa Watoto wenye ulemavu na wenye mahitaji maalumu.

Mnzava ametoa karipio hilo wakati akizindua Shule mpya ya Itonga iliyopo Bungu “A” na kusema mbali ya unyanyasaji pia wapo wanaoendelea kuwaficha watoto hao na kuwanyima haki zao za Msingi ikiwemo elimu na kuitaka jamii iwasimamie ili wapate haki zao.

Amesema, Serikali kwasasa inaendelea kuboresha mazingira wezeshi kwa watoto wenye mahitaji maalumu hivyo jamii nayo inatakiwa kuachana na tabia za kuwabagua.

“Nimeisikia hapa Serikali imekuwa ikitoa sh. Milioni 1.3 kila mwezi kwa ajili ya kupata chakula na mahitaji maalumu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu, tuendelee kusimamia mahitaji yao muhimu,” aliongeza Kiongozi huyo.

Awali akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Rufiji, Mkuu ya Kibiti Kanal Joseph Kolombo amesema Mwenge huo utakimbizwa km 83.7 ambapo utaifikia miradi ya maendeleo 15 yenye thamani ya shilingi Bililoni 2.4.

Mwamba anarudi tena nyumbani
Beida Dahane apewa Fainali Ligi ya Mabingwa