Kiungo wa kati wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain Vítor Machado Ferreira ‘Vitinha’ amesema ilikuwa vigumu kuzungumza baada ya kupigwa na Borussia Dortmund na kutupwa nje ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya usiku wa jana Jumanne (Mei 08).
Kichapo cha bao 0-1 ambacho kinatoa matokeo ya jumla ya 0-2, kinaendelea kudhihirisha, PSG hawana bahati ya katika kufikia lengo la Kutwaa Ubingwa wa Michuano hiyo mikubwa Barani Ulaya katika ngazi ya vilabu.
Vitinha alikuwa sehemu ya wachezaji wa PSG walionesha kupambana katika mchezo huo lakini PSG hawakuweza kupata bao, jambo ambalo lilimuacha mchezaji huyo kutoka nchini Ureno katika wakati mgumu wa kufikiria kwa nini walishindwa kutinga hatua ya Fainali.
“Ni ngumu kuzungumza kwa sasa, yalikuwa matokeo ya kukatisha tamaa, tulipambana na kujitoa kwa hali yote kama wachezaji lakini imeshindikana,” Vitinha aliiambia TNT Sports
“Sina mengi ya kuzungumza juu matokeo haya, lakini ninataka kuwashukuru mashabiki ambao walionesha kuwa na imani na timu yao wakati wote, ila hawakustahili matokeo haya. Ninaamini watafahamu kwamba tujitoa kwa ajili yao, ila haikutosha kuwafurahisha.”
“Sipendi kuhusisha kosa na bahati mbaya. Ninapenda kufikiria ni vitu vingine, katika mchezo wa kwanza na mchezo huu pia. Sitaki kabisa kufikiria juu hilo.” Vitinha alihitimisha