Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mbunge wa Jimbo la Babati mjini, Pauline Gekul amefanyiwa dua maalum katika Msikiti wa Taqwa uliyopo mjini Babati, wakati akiwa katika ziara yake iliyolenga kutimiza ahadi zake kwa Wananchi wa Jimbo lake.

Katika ziara hiyo na akiwa katika Msikiti huo, pia Gekul ametoa kiasi cha shilingi milioni 1.2 kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa msikiti huo na kutoa shilingi milioni 1 kwa UWT wilaya ya Babati mjini kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mtumishi.

Aidha, ametembelea ujenzi wa madaraja mawili yanayojengwa yenye thamani ya shilingi milioni 120 katika maeneo ya Chuo cha Uhasibu na mtaa wa Hangoni Wilayani humo ikiwa ni Moja ya ahadi zake alizotia kwa Wananchi wa Jimbo hilo mwaka 2023.

 

Katika hatua nyingine Gekul amekabidhi viti vyenye thamani ya milioni 2 kwa Wananchi wa mtaa wa Hangoni kwa matumizi ya Vikao na kuwataka kuvitunza, kuvilinda na kuwahimiza waendelee kuchapa kazi.

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo waendeleza vitendo
MAKALA: Ukiuheshimu utaratibu utakuheshimisha