Vyombo vya ulinzi na usalama Wilayani Kilosa vinamshikilia mtu mmoja Dotto Lusuka (21) huku vikiendelea kumsaka Suma Lusaka kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Lazaro Ndutu katika Kitongoji cha Kikuyu kilichopo Kijiji cha Kigunga, Kata ya Zombo, Tarafa ya Ulaya.

Akithibitisha kwa vyombo vya habari kuhusu mauaji hayo, Mkuu wa Wilaya hiyo iliyopo mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka amesema tukio hilo lilitokea asubuhi ya Mei 11, 2024 ndani ya hifadhi ya msitu wa kijiji hicho, ikisadikiwa kuwa chanzo cha ni ugomvi wa kuwania eneo.

Shaka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Wilaya, amesema Machi 2024 alipokea taarifa za Wananchi kuvamia msitu huo na Serikali ikachukua hatua za kupiga marufu uvamizi na kufanya doria kudhibiti vitendo hivyo.

Amesema, “tulipiga marufu na kuimarisha doria katika hifadhi za misituni baada kupata taarifa za uvamizi na kulielekeza Jeshi la Polisi, TFS na halmashauri kusimamia matumizi na kulinda hifadhi za misitu pamoja na juhudi kadhaa kuchukuliwa.”

Serikali yaridhia Juni 6, yasamehe kodi makusanyo ya Watalii
Udhibiti wahamiaji haramu: Ulinzi kuimarishwa mpakani