Mtangazaji mkongwe Shirika la Utangazaji Nchini – TBC, Ramadhani Swedy Mwinyi amefariki dunia.

Swedy amefariki hii leo Mei 12, 2024 katika Hospitali ya Mloganzila iliyopo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akitibiwa.

Ramadhani Swedy Mwinyi.

Atakumbukwa kwa umahiri wake na sauti yake adhimu katika utangazaji wa mpira wa miguu enzi za uhai wake.

Pumzika kwa amani Ramadhani Swedy Mwinyi.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 13, 2024
Serikali yaridhia Juni 6, yasamehe kodi makusanyo ya Watalii