Serikali Nchini, imesema inaangalia namna ya kupunguza gharama za uingizaji wa vifaa vya nishati safi ya kupikia ili kuwawezesha wananchi kumudu matumizi ya nishati hiyo ikiwemo ya gesi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amesema hayo bungeni leo Mei 13, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Santiel Kirumba aliyeuliza Serikali imejipangaje kuweka ruzuku katika nishati ya gesi ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
Amesema, ili kuhakikisha hatua hiyo, Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Nishati na Wizara ya Fedha zimekutana na kujadili namna ya kuwasaidia Wananchi kutumia nishati safi na kuacha kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa na kwamba mkakati wa Taifa umependekeza Wizara zinazohusika kuchukua hatua ya kupunguza gharama hizo, ili wananchi wazimudu.
Akijibu swali la Mbunge wa Kalenga, Jackson Kiswaga aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kupanda miti kando ya mito na barabara, Naibu Waziri Khamis amesema tayari Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wizara na taasisi mbalimbali inaendelea na mpango wa kupanda hususan mkoani Dodoma ili kurejesha miti yaa asili ili kutunza na kuhifadhi mazingira.
Awali, katika swali la msingi la Kirumba aliyeuliza Serikali imejipangaje kuhimiza wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira ikiwemo upandaji miti, Naibu Waziri Khamis amesema katika mwaka 2024/2025, Serikali imepanga kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa utunzaji, hifadhi na usimamizi wa mazingirakwa njia mbalimbali ikiwemo.