Mshambuliaji wa Arsenal, Kai Havertz ametangaza kuwa atakuwa shabiki mkubwa’ wa wapinzani wao Tottenham Hotspurs ili washikabunduki hao waweze kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England.

Kinyanganyiro cha kuwania taji hilo kitaenda hadi siku ya mwisho ya msimu baada ya vijana wa Mikel Arteta kushinda 1-0 dhidi ya Manchester United Juzi Jumapili (Mei 12) na kusonga mbele kwa pointi moja na Manchester City katika nafasi ya pili.

Hata hivyo, City bado wana mchezo mkononi wa kucheza na huo utakuja ugenini kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur leo Jumanne (Mei 14) kwenye uwanja ambao wamepoteza mechi zote za Ligi Kuu bila kufunga bao.

Havertz, ambaye alitoa pasi ya bao la ushindi kwa Leandro Trossard kwenye Uwanja wa Old Trafford, aliiambia Sky Sports kwamba anatumaini wapinzani wa Arsenal wa London kaskazini watawafanyia neema.

“Nitakuwa shabiki mkubwa wa Tottenham milele!” amesema

“Wacha tutegemee bora. Lazima tushinde kwani City wanazidi kuweka presha.”

“Inapendeza sana kuwa katika mbio za taji na kila wiki lazima ucheze kwa ubora wako. Unapofanya hivyo, unajisikia vizuri zaidi. Tuna mchezo mmoja na tunahitaji klabu nzima nyuma yetu chochote kinawezekana.

Tottenham wanawėza kuhitaji ushindi dhidi ya City ili kuweka hai matumaini yao ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao 2024/25.

Iwapo City watatoka sare na Tottenham, watakaa nyuma ya Arsenal kwa tofauti ya mabao pekee.

City watawakaribisha West Ham United siku ya mwisho, huku Arsenal wakiwakaribisha Everton kwenye Uwanja wa Emirates.

Juma Mgunda: Tunaitaka nafasi ya pili Ligi Kuu
Majaliwa: Mauzo ya nyama nje ya nchi yameongezeka