Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amesema inawezekana timu yake kutwaa taji la Ligi Kuu ya England ‘EPL’ msimu huu 2023/24.

Arteta ametoa kauli hiyo baada ya kikosi chake kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kufuatia ushindi wa bao 1-0 iliyoupata dhidi ya Manchester United, Uwanja wa Old Trafford, England juzi Jumapili (Mei 12).

Katika mechi hiyo, bao la Arsenal lilifungwa na Leandro Trossard akimalizia pasi ya Kai Havertz katika dakika ya 20.

Arsenal inaongoza ligi ikiwa na pointi 86 katika mechi 37, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 85 katika michezo 36.

Ili kutwaa taji hilo, Arsenal inapaswa kuiombea matokeo mabaya Man City itakapocheza na Tottenham leo Jumanne (Mei 14), huku ikitakiwa kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Everton wakati City itakapomalizana na West Ham United.

“Juzi tulitaka kufungua huo mlango. Mbele ya mashabiki wetu wacha tuishi moja kati ya siku nzuri zaidi ambazo tulizishi pamoja. Tutakaa tukitazama mchezo (kati ya Tottenham na Man City) na ni kweli tunahitaji matokeo ili kufanikisha hilo (kutwaa taj),” amesema Arteta

Kwa mujibu wa mtandao wa takwimu wa Opta, Arsenal ina asilimia 41.3 za kutwaa taji la Ligi Kuu England msimu huu wakati Man City ikiwa na asilimia 58.7.

Pamoja na Arsenal kuwa na matumaini ya kubeba taji hilo, lakini kiungo wa zamani wa Man United, Roy Keane amesema haoni uwezekano wa kuisimamisha Man City isitwae taji hilo.

Minziro achelekea sare Kaitaba
Utekelezaji maeneo saba ya vipaumbele Sekta ya Uvuvi