Katika mwaka 2023/2024, Sekta ya Uvuvi, imetekeleza maeneo saba ya kipaumbele ambayo utekelezaji wake umezingatia Dira ya Taifa (2025) ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III 2021/2022 – 2025/2026), ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi – CCM.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2024/2025 Bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema pia wataifungamanisha Sekta na dhana ya Uchumi wa Buluu, hususan matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi ikiwemo kwenye maji ya asili na ukuzaji viumbe maji.
Amesema, “utekelezaji wa vipaumbele hivi umewezesha Sekta kupata mafanikio na matokeo ya Kufanya mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni za Sekta ya Uvuvi,Kuimarisha taasisi za uvuvi ili kuongeza ushiriki katika Uchumi wa Buluu, Kuimarisha uwezo wa uvuvi katika bahari kuu, Kuimarisha ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi.”
Ulea ameongeza kuwa, “lakini pia Kuongeza uwekezaji katika miundombinu ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji, Kuimarisha uthibiti wa ubora wa mazao ya uvuvi na masoko na Kuimarisha huduma za ugani wa uvuvi na ukuzaji viumbe maji.”
Hata hivyo, amesema katika mwaka 2023/2024, Wizara imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uvuvi ya Mwaka 2015 kupitia sheria na kanuni mbalimbali za Sekta ya Uvuvi.
“Pia Wizara imeandaa rasimu ya Kanuni za Ukuzaji Viumbe Maji ambayo imepitiwa na wadau mbalimbali na tayari rasimu hiyo imewasilishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa uhakiki na kupata maoni yake.,Vilevile, Wizara inaendelea na mapitio ya Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009,” amesema Ulega.
Katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali za uvuvi Wizara imekamilisha andiko la kuanzisha Mamlaka ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji ambayo itakuwa na jukumu la kuendeleza, kusimamia, kudhibiti na kuhifadhi rasilimali za uvuvi na ukuzaji