Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Fred Felix Minziro amesema amefurahishwa na namna wachezaji wake walivyopambana kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu juzi dhidi ya Simba SC na kufanikiwa kuondoka na pointi moja.

Minziro amesema matokeo hayo yataongeza hamasa kwa wachezaji wake kuelekea kwenye mchezo ujao dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Mei 21.

Minziro amesema wachezaji wake walifuata malekezo yake kwenye mchezo dhidi ya Simba SC na kufanikiwa kuwabana wapinzani wao hao wasiondoke na pointi zote tatu.

“Wakati wa mapumziko niliwaambia wachezaji wangu waende wakapambane, tunao huo uwezo wa kupambana, niliwapa na maelekezo mengine ya kifundi na kweli walipambana na kufanikiwa kusawazisha goli,” amesema Minziro

Amesema kwa sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo unaofuata ambao nao watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri waweze kutoka sehemu walipo sasa kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

“Kwa sasa kila mchezo ni mgumu, imebaki michezo michache na kila timu inataka kupambana kupata matokeo mazuri ili kujiweka katika nafasi nzuri kabla ligi haijamalizika, hata mchezo na Coastal Union hatutegemei kuwa mwepesi, utakuwa mchezo mgumu lakini tutapambana kama tulivyofanya kwa Simba SC,” amesema Minziro

Matokeo ya juzi Jumapili (Mei 12) yameifanya Coastal Union kufikisha pointi 30 na kushika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza michezo 26 mpaka sasa wakiwa wamebakiza michezo miwili kumaliza ligi.

Watanzania kukipiga na Tottenham, Wolves
Arteta anasubiri hatma ya ubingwa EPL