Neymar amesema ana hamu kubwa ya kurejea uwanjani baada ya kusherehekea taji la Al Hilal la Saudi Pro League (SPL) na wachezaji wenzake siku ya Jumamosi.

Kikosi cha Jorge Jesus kilifanikiwa kunyakua taji lao la 19 la ligi lililoongeza rekodi siku ya Jumamosi kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hazem na kuwafanya wabaki na pointi 12 mbele ya Al Nassr ya Cristiano Ronaldo ikiwa imesalia mechi tatu kumalizika kwa msimu.

Nyota huyo kutoka nchini Brazil aliahidi furaha msimu ujao huku akiwamwagia sifa wachezaji wenzake.

“Nina furaha sana bila shaka. Kushinda mataji siku zote ni vizuri. Jambo bora zaidi lingekuwa uwanjani, lakini nina furaha sana kwa wachezaji wenzangu.”

Neymar alisema: “Niko sawa. Najisikia vizuri. Nina hamu kubwa kurejea uwanjani.

“Kwa bahati mbaya, sijaweza kuwapa furaha wanayostahili lakini unaweza kuwa na uhakika kwamba msimu ujao tutakuwa na furaha nyingi.”

Neymar mwenye umri wa miaka 32, aliichezea Al Hilal mechi tatu pekee za SPL kabla ya kuumia Oktoba na kufanyiwa upasuaji muda mfupi baadaye.

Dabo: Ninaitaka nafasi ya pili Ligi Kuu
Uzoefu kumbeba Kakolanya Young Africans