Arsenal huenda ikaangukia pua katika mchakato wa kuwania saini ya Mshambuliaji wa Newcastle United, Alexandre lsak baada ya Liverpool kuonyesha nia ya kutaka kumsajili Antony Gordon kutoka hapohapo Newcastle.
Kwa mujibu wa Daily Star, ikiwa Liverpool itafanikisha mchakato wa kumsajili Gordon kuna uwezekano mkubwa Newcastle ikasitisha mpango wa kumuuza lsak kwa sababu itakuwa imeshajiweka salama na sheria za matumizi ya pesa.
Kwa sasa Newcastle ambayo imetumia pesa nyingi kwenye usajili na mishahara ndani ya misimu hiyo miwili, inaweza ikapata adhabu kutoka mamlaka za soka za England na UEFA kwa kukiuka sheria za matumizi ya pesa, ambapo inatakiwa kutumia kulingana na inachoingiza.
Katika kupambana na hilo imedhamiria kuuza mchezaji mmoja staa ambaye atawapa pesa nyingi zikatazoweza kuwafanya wasajili bila wasiwasi na miongoni mwa mastaa hao ni Isak na Gordon.
Hivyo ikiwa Liverpool itaweka pesa nyingi na kumsajili Gordon, Newcastle itaacha kumuuza lsak.