Afisa Masoko Hifadhi za Bahari Tanzania, Halima Tambwe amesema Hifadhi ya Bahari Tanzania ambayo ipo chini ya Wizara ya mifugo na Uvuvi inaendelea kuitangaza Tanzania na kupokea idadi kubwa ya watalii kutoka mataifa mbalimbali Duniani.

Kwa mwaka 2024 kuanzia mwezi wa pili hadi wa nne wameweza kupokea watalii zaidi ya 460 ikiwa ni matokeo mazuri ya Tha royal tour

Akizungumza na Dar24 Media hii leo Bungeni Jijini Dodoma amesema kwa mwaka 2024 kuanzia mwezi wa pili hadi wa nne wameweza kupokea watalii zaidi ya 460 ikiwa ni matokeo mazuri ya ‘The royal tour’.

Afisa Masoko Hifadhi za Bahari Tanzania, Halima Tambwe.

 

Amesema, “tunamshukuru sana Rais kwa kuwa amekuwa ni miongoni mwa watu wanao utangaza utalii wetu kwa asilimia kubwa sana hasa katika sekta hii ya Bahari.”

“Na haya yote ni matokeo ya The royal tour ya Rais wetu, yeye ndio amekuwa tour guide Mkuu katika hili, na mpaka mwaka huishe najua tutapokea watalii wengi zaidi.” amesema Tambwe.

Bruno Fernandes kung’oka Old Trafford
Chirwa: Nimewajibu kwa vitendo