Uongozi wa Klabu ya Bayern Munich inafirikia kumng’oa Kiungo kutoka nchini Ureno Bruno Fernandes kwenye klabu ya Manchester United, ili kuboresha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Ujerumani.
Fikra za kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 zinapewa kipaumbele huko Allianz Arena, kufuatia Man Utd kuwa tayari kupokea ofa.
Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Gazeti la Independent ambalo mapema leo Jumatano (Mei 15) limeripoti kuwa Fernandez yupo tayari kuondoka Old Trafford na kwenda kusaka changamoto mpaya.
Fernandez amekuwa akicheza vyema katika kikosi cha Erik ten Hag msimu huu licha ya United kukabiliwa na uwezekano wa kukosa nafasi ya kucheza Michuano ya Uropa msimu ujao 2024/25.
Gazeti la Independent limeandika: “Bayern Munich inajipanga kumsajili Bruno Fernandes mwishoni mwa msimu huu, Klabu hiyo inaamini kuwa inaweza kumpata kutokana na kuzidi kukasirishwa na Manchester United,”
“Pia kuna hisia kwamba uongozi wa Manchester United utakuwa tayari kufanya makubaliano, kwa kuwa wanahitaji kuuza wachezaji ili kukidhi mahitaji ya Kanuni ya Matumizi ya fedha ‘FFP’.”
“Uhamisho kama huo unaweza pia kuwa ishara ya mafanikio katika kumbakisha Thomas Tuchel katika klabu hiyo ya mjini Munich, kwani alitaka mchezaji mwingine mbunifu msimu huu na Mreno huyo analingana na wasifu wake.”
“Bayern wanataka kubadilisha mtyazamo wa kikosi chao huku wakilenga kuboresha safu ya Kiungo na Ushambuliaji, na Fernandes ni chaguo sahihi kwa sasa.”