Kocha Mkuu wa Klabu ya Brentford Thomas Frank anatajwa kuwa mshindani mkuu katika kinyang’anyiro cha kumrithi Kocha Mkuu wa Man Utd Erik ten Hag.
Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph, Frank anaonekana kuwavutia viongozi wa Man Utd, huku ikielezwa Ten Hag ana nafasi finyu ya kuendelea kusalia klabuni hapo.
Ten Hag anakabiliwa mazingira magumu ya kazi huko Old Trafford, huku timu hiyo ikiwa katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, ingawa wametinga Fainali ya Kombe la FA ambapo watacheza dhidi ya Manchester City.
Iwapo uongozi utaamua kumfukuza Kocha huyo kutoka nchini Uholanzi, ripoti zinaonyesha kuwa Kocha Frank anaweza kuwa katika nafasi ya kuchukua nafasi ya kuliongoza Benchi la Ufundi pale Old Trafford.
“Thomas Frank anaongoza katika ushindani wa kazi katika Klabu ya Manchester United ikiwa Uongozi utabadilisha Kocha kufuatia changamoto za kilabu hiyo chini ya Erik ten Hag,” imeeleza taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la The Telegraph
“United bado hawajafanya uamuzi juu ya mustakabali wa Ten Hag, ambaye bado anaweza kushinda Kombe la FA mwaka huu, lakini Kocha Frank anaendelea kutajwa kama chaguo la kwanza huko Old Trafford kutokana na kazi yake nzuri anayoifanya Brentford.
“Kocha huyo wa Denmark ana uhusiano uliopo na wamiliki wenzake Ineos na amewahi kuungana na Sir Dave Brailsford, mkurugenzi wa michezo katika kampuni hiyo, kabla ya kuwekeza United kwa kuhudhuria chakula cha jioni cha miaka 60 mwezi Machi pamoja na Sir Alex Ferguson, Arsene Wenger, Roy Hodgson na meneja wa Chelsea Mauricio Pochettino.
“Inafikiriwa kuwa Kocha huyo atafaa katika muundo mpya wa United kufuatia mmiliki wa Ineos Sir Jim Ratcliffe kuchukua udhibiti wa uendeshaji wa soka.”