Gwiji wa Manchester United, Wayne Rooney, amewashutumu wachezaji wa kikosi cha Erik ten Hag kwa kujificha nyuma ya majeraha na kuchagua kutoshiriki katika timu yao mwishoni mwa msimu huu.

Ukosoaji wa mshambuliaji huyo wa zamani umekuja baada ya United kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Old Trafford, wakati ambapo kocha Ten Hag alilazimika kukabiliana na wachezaji wengi waliokosekana huku Marcus Rashford na nahodha Bruno Fernandes wakishindwa kujumuishwa kwenye kikosi.

Kukosekana kwao kunaongeza orodha inayoongezeka ya wachezaji majeruhi wa United, huku Mason Mount, Harry Maguire, Luke Shaw, Raphael Varane, Lisandro Martinez, Victor Lindelof, Tyrell Malacia na Anthony Martial wakiwa nje kwa sasa.

Rooney alikuwapo kwenye mechi ya Jumapili (Mei 12) waliyopoteza Old Trafford, alitoa mawazo yake kuhusu shida va timu yake ya zamani.

Akizungumza na Sky Sports alisema: “Kikosi kina wachezaji wazuri sana lakini uchezaji wao uko chini ya kiwango, tukiangalia majeruhi waliopoa bado baadhi ya wachezaji waliopo wanaweza kucheza kwa asilimia 100.

“Kama wako nyuma ya Ten Hag hawaoneshi vizuri sana. Ni rahisi unapokuwa na Ubingwa wa Ulaya au fainali ya Kombe la FA, kwa wachezaji kukaa nje kwa muda kidogo kisha wajiandae na fainali na Euro 2024.

“Nimejionea hili kwa miaka mingi na nadhani wachezaji hawajijazi na sifa yoyote kwa sasa na makocha wanawajibika kwa hilo.”

Kocha Geita Gold akata tamaa Ligi Kuu
Mgunda aipongeza Young Africans, akomaa na Chasambi, Balua