Baada ya kukaribia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, Simba Queens inataka kumaliza msimu huu bila ya kufungwa mechi hata moja.

Kocha Mkuu wa Simba SC Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’ amesema anataka kushinda mechi zote zilizosalia na hatawadharau wapinzani wao kwa sababu anataka kuweka rekodi ya kutopoteza mchezo.

Mgosi amesema wanaheshimu kila timu wanayocheza nayo na kwao kila mechi ni sawa na fainali.

“Tunataka kushinda mechi zote, tunataka kumaliza msimu na rekodi nzuri, hatutabweteka, tunataka kushinda michezo iliyobakia, tunaendelea kujipanga ili kuhakikisha tunafikia malengo,” Mgosi amesema

Bingwa Wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania ataiwakilisha Bara katika mashindano ya kimataifa ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’, yatakayofanyika baadae mwaka huu.

JKT Queens ya Tanzania Bara ndio ilikuwa inashikilia ubingwa wa CECAFA ambao iliwavua Simba SC Queens msimu uliopita, lakini Maafande hao waliishia hatua ya makundi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake.

Ubovu wa miundombinu kero soko la Mawenzi Moro
Kocha Geita Gold akata tamaa Ligi Kuu