Kufuatia madai ya vipigo na adhabu kali kwa Wafanyabiashara wasiolipa ushuru, Serikali imesema haitavumilia ukiukwaji sheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya Watumishi watakaobainika kukiuka sheria kwenye ukusanyaji mapato.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Mei 15, 2024 Bungeni jijini Dodoma, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa wakati akitoa ufafanuzi wa malalamiko yaliyotolewa na Mbunge wa Msalala – CCM, Idd Kassim.

Malalamiko ya Mbunge Kassim yaliyotolewa Bungeni wiki iliyopita akidai kuwa Mamlaka za Seikali za Mitaa zinatoza ushuru mashambani na Wafanyabishara wasiolipa wanapewa adhabu kali ikiwemo kupigwa.

Akifafanua jambo hilo, Mchengerwa amesema ushuru wa mazao hutozwa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290 na vifungu vya 6,7,8 na 9 vya sheria hiyo ushuru wa mazao ni moja ya vyanzo vya mapato kwa mamlaka za miji, halmashauri za wilaya, mamlaka za miji midogo na halmashauri za vijiji.

Amesema, kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa,Sura ya 290 ushuru huo unatozwa kwa asilimia tatu ya bei ya kununulia shambani kwa mazao ya chakula na biashara.

Postecoglou: Saa 48 zimenifunza mengi
MAISHA: Akili yenye uwezo mkubwa wa kufikiri