Mkuu wa mkoa manyara, Queen Sendiga amewataka Wakala wa Maji na Uusafi Mazingira – RUWASA, kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora ya Maji safi na salama muda wote.

Ameyasema hayo katika kikao cha Watumishi wa RUWASA Mkoani humo kilicholenga kuwajengea uwezo watumishi hao katika Kutoa huduma Bora za maji kwa wananchi wa vijijini.

Amesema, RUWASA, Mkoa wa Manyara imeendelea kutimiza azma yake ya utekelezaji wa agizo la Rais Dokta Samia Suluhu Hassan la kumtua ndoo mama kichwani kwa kuwahudumia Wananchi kwa maji safi na salama na kufikisha asilimia 70.5 mwaka 2023.

Awali, Meneja Wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Manyara, Walter Kirita alitangaza dhamira hiyo katika kikao kazi cha watumishi wa RUWASA mkoa wa Manyara kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya White Rose Wilayani Babati.

Ameisema, RUWASA wakati inaanzishwa upatikanaji wa maji ulikuwa ni asilimia 55.5 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 70.5 Disemba 2023 ambapo kufuatia miradi ya maji inayoendelea kiwango hicho wanaimani kuwa kitaongezeka.

“Ukuaji huu imara wa kumtua ndoo mama kichwani ni matokeo ya ushirikiano baina ya RUWASA na viongozi wa mkoa wa Manyara kwa kufuata Sheria na kanuni ambazo ni rafiki kiutendaji kwa watumishi wa RUWASA na wananchi,” alisema Kirita.

Aidha, alifafanua kuwa kwa kufanyakazi kwa pamoja kutaleta ufanisi na kutatua changamoto za kiutendaji zitakazosaidia kufikia malengo kupitia bajeti iliyopitishwa ya Bilioni 19.9 ya Wizara hiyo kiasi ambacho kitawafikisha utekelezaji wa miradi ya malengo waliojiwekea.

Azma hiyo, imekuja wakati Dunia ikisheherekea siku ya familia duniani tarehe 15 Mei ya kila mwaka yenye lengo la kukumbusha wajibu wa kulea familia sambamba na umuhimu wa upatikanaji wa maji kwa familia.

Naye Meneja Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu RUWASA, Philomena Luambano alisema Taasisi hiyo itaendelea kufanyakazi kwa kuzingatia ilani ya CCM inayotamka kumtua ndoo mama kichwani.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Mariam Muhaji alisisitiza watumishi hao kufuata miongozo ya utendaji kazi katika suala la ufundi,ununuzi wa vifaa usiogubikwa na vitendo vya rushwa.

Mwisho wa ubishi Usyk Vs Tyson Fury
Ubovu wa miundombinu kero soko la Mawenzi Moro