Mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Jimbo la Lupembe, Edwin Swale ameliomba jeshi la Polisi kupanga mikakati mizuri ya kulinda usalama wa mtandao.

Swale ameyasema hayo hii leo Mei 15, 2024 Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani na kudai kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinauwezo wa wa kudhibiti wizi wa mtandaoni kwa asilimia zote.

Amesema, “wizi wa mtandao dunia unakwenda mbele sana, zamani wizi ulikuwa unafanyika kwa kutumia nguvu lakini sasa hivi wanatumia mitandao katika kufanya uwizi huo, naomba Jeshi la Polisi wapange mikakati ya kulinda usalama wa mtandao.”

Hata hivyo, katika hatua nyingine Mbunge Swale ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani katika bajeti hii ya fedha, wawasaidie waendesha Bodaboda kupunguziwa bei ya Leseni.

New Post
Serukamba azionya Taasisi zisizotumia mfumo wa NeST