Wawakilishi wa SSC Napoli walikutana na Antonio Conte mjini Turin, wakati AC Milan wanaonekana kama hawana nia tena ya kumchukua kocha huyo kutoka nchini Italia.
Inadaiwa SSC Napoli ilikutana na Conte huko Turin, ikimuahidi ofa kocha huyo wa zamani wa Juventus na Inter Milan kiasi cha Euro milioni 6.5 (sawa na Sh Bilioni 18) ikiwa ni kiwango cha mshahara wake wa mwaka pamoja na nyongeza endapo watafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao 2024/25.
Ikiwa Conte atakubali ofa hiyo, atapata Bonsai ya Euro milioni 2 (sawa na Sh Bilioni 5) ambayo itaongezwa katika mshahara wake kuanzia msimu wa mwaka 2025- 26, kwa mujibu wa ripoti.
Mitandao inadai Conte ni chaguo la kwanza la SSC Napoli kwa msimu ujao 2024/25.
Kinyume chake, La Gazzetta dello Sport limedai Partenopei inamtaka Stefano Pioli huku Corriere dello Sport ikisema SSC Napoli itasubiri mwisho wa msimu ili kuanza mazungumzo na Gian Piero Gasperini wa Atalanta.