Lydia Mollel – Morogoro.

Jeshi la polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kumtia mbaroni Samsoni Uwingirimanya (35), dereva na raia wa nchi ya Rwanda ambaye aliondoka eneo la tukio mara baada ya kusababisha ajali iliyotokea Mei 14, 2024 na kuua watu saba.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP, Alex Mkama amesema mtuhumiwa huyo amekamtwa akiwa amejificha kwenye nyumba ya wageni iliyopo Dumila, Wilayani Kilosa.

Katika hatua nyingine  Kamanda Mkama amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kuripoti matukio ya kihalifu yanayotokea kwenye maeneo yao.

Salahange Jela miaka 30 kwa kumbaka bintiye
Taarifa hali ya Dawa za kulevya yawasilishwa Bungeni