Serikali Nchini, ipo katika maandalizi ya usimami wa mikopo ya asilimia 10 kwa kuamua kuanzisha kitengo maalumu cha usimamizi wa Mikopo hiyo kwa ngazi ya Wizara, na kamati ya usimamizi wa mikopo katikati ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Kata.
Ameyasema hayo Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Zainabu Katimba Bungeni Jijini Dodoma hii leo Mei 17, 2024 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Christina Christipher Mnzava.
Mnzava alitaka kujua je, Serikali imejipanga vipi katika usimamizi wa mikopo ya asilimia 10, pindi itakapoanza kutolewa tena kuanzia Julai mosi?
Akijibu swahi hilo, Katimba amesema, “timu iliundwa kufanya mapitio na kuhakikisha unatengenezwa utaratibu bora zaidi kwa ajili ya kuhakikisha Mikopo, hii inatoka na inaenda kuwanufaisha walengwa na tayari katika Muundo wa usimamizi wa mikopo hii.
Amesema”kutaanzishwa Kitengo cha usimamizi wa Mikopo katika ngazi ya Wizara Ofisi ya Rais TAMISEMI na kamati za usimamzizi wa Mikopo katika ngazi ya Mikoa, Halmashauri na Kata, mikopo hii inayotokana na Mapato ya ndani ya Halmashuri, ilisitishwa kutokana na maelekezo ya Serikali ya kuangalia upya utaratibu na changamoto zilizokuwepo.