Shirika la Haki Rasilimali nchini Tanzania, limekamilisha utafiti uliokuwa unaangazia kwa kina mradi wa LNG, kimazingira, kijamii, kiuchumi, na sera, kwa kutathmini fursa na changamoto mbalimbali zilizopo.

Utafiti huo uliowasilishwa jijini Dodoma, ulilenga kutoa ufahamu na mapendekezo muhimu, ili kuelekeza mhamo wa nishati ya Tanzania kwa njia inayowajibika kulingana na ahadi za kimataifa.

Baadhi ya wabunge wanaowakilisha kamati mbalimbali ikiwemo ya Nishati na Madini, Katiba na Sheria walisema utafiti huo umekuja kwa kuchelewa na tayari jitihada mbalimbali zimeshachukuliwa na Serikali.

Kwa mujibu wa utafiti huo, idadi kubwa ya watu wameilalamikia sekta ya kilimo na kwamba uhamishaji umewalazimisha kubadili kilimo kwa kupanda Mtama na Mahindi, ambayo hayastawi vizuri katika maeneo yao mapya wanayoyafanyia kazi.

Kilimo ni mojawapo ya shughuli za mwanadamu ambayo humsaidia kupata mazao kwa ajili ya chakula na biashara ambayo inaweza kumuingizia kipato kwa ajili ya maisha yake na kukuza pato la Taifa.

Serikali kukamilisha mabadiliko sera ya Wazee - Gwajima
MALIMWENGU: Ukitanguliza mhemuko imekula kwako