Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda amesisitiza kuwahitaji zaidi Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kuelekea kwenye mchezo wa kesho Jumanne (Mei 21), utakaowakutanisha na Geita Gold FC.

Simba SC inayowania nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya Young Africans kujihakikishia Ubingwa watatu mfululizo, itakuwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam ikichagizwa na ushindi wa 0-1 iliyoupata kwenye mpambano uliopita dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano maalum wa kuzungumzi mchezo dhidi ya Geita Gold FC, Mgunda amesema Mashabiki na Wanachama wanapaswa kuendelea kuwa kitu kimoja na kuiunga mkoni timu yao, ambayo bado ina wahitaji katika kampeni za kufikia malengo waliyojiwekea kwenye kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimi huu 2023/24.

“Maandalizi ya kucheza mchezo mgumu wenye ushindani dhidi ya Geita Gold kwa ujumla wake yanakwenda vizuri, tupo tayari kushindana katika mchezo wa kesho na In Shaa Allah tutapata matokeo mazuri.

“Ninachowataka Mashabiki na Wanachama ni kuhakikisha wanakuwa pamoja na timu yao wakati wote, pamoja na kukiandaa vizuri kikosi changu, bado ninamuhitaji mchezaji wangu muhimu sana anayecheza namba 12 ambao ni Mashabiki na Wanachama wetu, kwa hiyo ninaamini wao wakitimiza wajibu wao na wachezaji wangu wengine 11 wakifanya yao, tutafikia lengo la kuibuka na ushindi kesho dhidi ya Geita Gold.” amesema Mgunda

Simba SC kwa sasa imefikisha alama 60 sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na uwiyano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Wenye mashaka, changamoto za vipimo waitwa WMA
Mzee ahofia Ziwa Victoria kuumeza Mkoa wa Kagera