Boniface Gideon, Muheza – Tanga.

Shirika la Mwambao Coastal Community Network kwa kushirikiana na Halmshauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, wamezindua rasmi kampeni inayoitwa ‘MKUBA’, ikiwa ni Mkakati wa Kutunza Bahari.

Kampeni hiyo, inalenga kuhamasisha na kuiwezesha Jamii Kutunza Bahari kwakupunguza shughuli za kibinadamu na kulinda rasilimali za viumbe hai vinavyoizunguka Bahari,huku Wakazi wa maeneo husika wakiwezeshwa kiuchumi.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanywa  na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Muheza, Stella Kategiro katika fukwe za Bahari ya Kijiji cha Kigombe, iliyoenda sambamba na kukabidhi fedha Sh. 10.5 Mil kwa vikundi 5 vya Wajasiriamali zilizotolewa na Shirika hilo.

Stella aliwataka Wakazi wanaoishi Mwambao wa Bahari kuacha tabia ya kufanya uharibifu wa rasilimali za viumbe hai Bahari ili kuongeza uzarishaji wa Samaki.

Alisema, “mnakata mikoko pia mnavua Samaki kwa uvuvi haramu,acheni hizo tabia, tunataka tuongeze kiwango cha uzarishaji wa Samaki mana wanazidi kuadimika, lakini pia tunatakiwa tupande mikoko na Kutunza fukwe kwakuacha kutupa taka ngumu ambazo ni sumu kwa viumbe hai wa majini zikiwemo chupa na mifuko ya plastiki.”

Aidha, katika hatua nyengine Stella, aliwataka wanufaika wa Fedha zilitolewa na wahisani kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa,
“hizi fedha zilitolewa na wenzetu wa Mwambao Coastal Community Network Tanzania, naomba tuzitumie kwa malengo yaliyokusudiwa, msije mkaenda kugawana kununua vijora,tunahitaji fedha hizi zizarishe na ziongeze kipato cha kila mmoja wetu hapa” Aliongeza Stella

Wanachama wa vikundi vya Kutunza Bahari kata ya Kigombe, wakiwa katika picha ya pamoja.

Kwaupande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwambao Coastal Community Network Tanzania, Said Khalid alisema “fedha hizi tunazozitoa ni sehemu ya mpango kazi wetu wa kuinua kiuchumi Wakazi wanaoishi Mwambao wa Bahari, tunatoa Elimu ya utunzaji rasilimali za viumbe hai Bahari,kuwawezesha kielimu,Nyenzo na fedha kwa Jamii inayozunguka Bahari ili waongeze uzarishaji wa Samaki.”

Alisema kwa Mkoa wa Tanga,mpaka hivi sasa, Vijiji 20 kwenye kata 17 na vikundi 103 vyenye Wanachama 3027 kati yao Wanawake 2119 na Wanaume 908 wamenufaika na Mradi huo wa ‘MKUBA’,

Dkt. Tax: Wizara kufanya tathmini hali ya mafunzo JKT
Wenye mashaka, changamoto za vipimo waitwa WMA