Lydia Mollel – Morogoro.

Ubovu wa miundombinu ya barabara imekua kero kubwa kwa wakazi wa Kiwanja cha ndege pamoja na Wafanyabiashara wa soko la Mawenzi Manispaa ya Morogoro, kwani unakwamisha shughuli za kijamii katika eneo hilo.

Wakizungumza na Dar24 Media kwa nyakati tofauti Wakazi wa eneo hilo wamesema ni takriban mwaka sasa tangu barabara hiyo kuharibika licha ya mvua iliyokuwa ikinyesha kuongeza uharibufu zaidi.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara katika soko la Mawenzi, Ramadhani Mohamed ameeleza kuwa changamoto kubwa katika soko hilo ni miundombinu ya barabara na tayari wameliwasilisha kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro na kuhaidi kufanya marekebisho katika soko hilo.

“Hili tulishalisemea mara nyingi tumeshakwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Wakurugenzi waliopita kwasababu Wakurugenzi huwa wanaamishwa na Wakurugenzi wote walioamishwa changamoto hii wameiacha na sasa ivi Mkurugenzi aliepo maelezo anayotoa ni kwamba kuna bajeti iliyotengwa kwajili ya ukarabati mkubwa wa soko letu,” alisema Mohamed.

Mshtahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga amesema tayari wameshatenga bajeti ya fedha shilingi milioni 700 kwa ajili ya kununua greda moja itakayotumika kutengeneza barabara zote zitakazokuwa zikiaribika hadi kufikia mwishoni wa mwezi juni, kwani kero wanazokutanazo wananchi zinawaumiza watumiaji wote barabara hizo ikiwemo yeye mwenyewe.

 

 

“Watumiaji wa barabara ni wananchi hawa wa kwangu mimi kama meya wa manispaa ya Morogoro kwahiyo maumivu wanaopata maumivu ni  mimi pamoja na wananchi wangu, sasa sisi kama viongozi wa manispaa kwa maana ya Baraza la Madiwani tukaona fedha hizi tunazokusanya kwa ajili ya maendeleo tutenge kiasi fulani tuweze kupata mtambo mmoja kwa maana ya Greda,” alisema Kihanga.

Mafuriko: Sillo awatembelea Wakazi waliokosa pa kuishi, chakula
Simba SC hakuna kukata tamaa