Klabu za Manchester City na Newcastle zimeingia vitani kuisaka saini ya Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ureno na klabu ya Wolverhampton Wanderers Pedro Lomba Neto.

Taarifa ziliochapishwa kwenye gazeti la Telegraph mapema leo Jumanne (Mei 21) zinaeleza kuwa, klabu hizo zimedhamiria kumsajili Kiungo huyo kutokana na kuridhishwa na kiwango chake kwa msimu wa 2023/24.

Hata hivyo Gazeti hilo limesisitiza kuwa lakini Uongozi wa Klabu ya Wolverhampton Wanderers umetangaza kuwa tayari kumuachia Neto, kwa sharti la kupokea Pauni Milioni 60 kama ada yake ya usajili.

Wolverhampton Wanderers inahitaji kumuuza Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa kiasi kikubwa cha fedha, ili kumuwezesha Kocha Gary O’Neil kuunda upya kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25.

Gazeti la The Telegraph limeandika: ” Wolverhampton Wanderers hawana shinikizo la kutafuta pesa ili kuepuka kukiuka kanuni za kifedha ‘FFP’ msimu huu wa usajili, baada ya mauzo yao ya Pauni Milioni 140 kwa mwaka jana.

“Matheus Nunes, Ruben Neves, Raúl Jiménez, Nathan Collins na Conor Coady waliuzwa msimu uliopita wa joto huku Wolverhampton Wanderers wakichukua hatua kali kuzuia kuvunja kanuni za kifedha ‘FFP’.

“Hata hivyo kocha mkuu Gary O’Neil amedhamiria kuunda upya kikosi chake kabla ya msimu ujao, huku Neto akiwaniwa na klabu za Man City na Newcastle United.

“Licha ya msimu wa winga huyo kutatizwa na majeraha ya nyama za paja, Neto bado alimaliza msimu wa 2023/24 akiwa na mabao mawili na asisti tisa.”

Pauni Milioni 25 kumng’oa Chalobah
Arne Slot akabidhiwa mikoba Liverpool